Kuhusu blog hii

Ngao ya Uhuru (Nembo ya Taifa)

UTAMADUNI NI NINI?

Sera ya utamaduni ya 1997 inaelezea maana ya  utamaduni kuwa ni “jumla ya mambo yote yanayobuniwa na jamii ili kukidhi utashi na maendeleo yake. Kwa maneno mengine, utamaduni ni mwenendo wa maisha ya jamii, mtazamo wao wa mambo, na taratibu zao za kuendesha maisha zinazowatofautisha wao na jamii nyingine. Utamaduni ndicho kitambulisho kikuu cha taifa na ni kielelezo cha utashi na uhai wa watu wake. Kwa hiyo basi umoja, utulivu na mshikamano ambavyo Watanzania wanajivunia vinatokana na utamaduni tuliojijengea. Nguzo za utamaduni huu ni pamoja na mila na desturi, lugha, sanaa, michezo na historia yetu.

Kwa kuwa utamaduni nchicho kitambulisho KIKUU  cha taifa na KIELELEZO cha  UTASHI  na  UHAI  wa WATU wake, blog hii inalenga kujadili  masuala mbalimbali yahusuyo utamaduni wetu hasa wa mtanzania. Jinsi watanzania wanavyouchukulia utamaduni wao, lakini pia Serikali na viongozi wake. Inalenga pia kuonesha mambo mbali mbali ya kiutamaduni yaliyokwenye nchi yetu ilikusaidia kukuza utalii wa kiutamaduni  (Cultural Tourism) nchini, inilenga kuwa sauti ya wasanii wote wa kitanzania walioko kila mahali  hasa wale wenye juhudi katika kukuza na kuuendeleza utamaduni wetu.  Ni sehemu ambapo maafisa utamaduni wote wa ngazi zote wataweza kutoa maoni yao na elimu kwa umma wa watanzania kuhusu umhimu wa kuujali na kuutunza utamaduni wetu.

Ili tuweze kufikia malengo ya Taifa kama yalivyo hainishwa katika Dira ya Taifa 2025, yaani Maisha bora, Amani, mshikamano na umoja, utawala bora, jamii iliyoelimika vema na yenyekujifunza pamoja na uchumi imara wenye ushindani, lazima jamii yetu iujue utamaduni wake na kuulinda!

KARIBU TUJADILI, TUELIMISHANE, TUKOSOANE JUU YA UTAMADUNI WETU

1 Comment (+add yours?)

  1. Hadji Selemani
    Jun 18, 2012 @ 12:00:51

    Sawia Kabisa Kwa Kila Kitu Mnachokifanya na Nimefurahia Sana Kwa Kutilia Mkazo Wa Kudumisha Utamaduni Wetu Japokuwa Umagharibi ( Utandawazi ) Unachochea Kuharibu Na Kufifisha Mila Na Desturi Zetu.Ni Hayo Tu Kwa Leo Ila Safari Ijayo Tutachangia Juu Ya Njia Za Kuzuia Utandawazi Kumomonyoa Na Kuharibu Tamaduni Zetu . Ni Mdau Kutoka Tumaini Iringa University Nachukua Degree Ya Cultural Anthropology And Tourism.

    Reply

Leave a comment